NGUVU YA MSAMAHA







NGUVU YA MSAMAHA

​Endeleeni kuvumiliana na kusameheana kwa hiari ikiwa yeyote ana sababu ya kulalamika juu ya mwenzake." Sisi sote hujikwaa mara nyingi.”kumbuka
Upendo hufunika maovu yetu megi hasa pale yanapojitkeza mapungufu yetu.

                                     
        Hari ya kutokusamehe,
      Humfanya mtu kua katika 
      Hali ya unyoge
      Na mara nyigi hua
      Hawachelewi
      Kua na maswali yafuatayo: 
                                                          1. Ivi kwann nifaniwe hivi?  
                                                          2. Kwa nini mimi tu!?
                                                          3. Kwa nini wengina 
                                                              hayawakuti?
 
Mpaka wengine hujikuta wakienda mbari kiasi cha kukufulu. na wanasahau kua shida na matatizo ni kwa kila mmoja.
            
Namshukuru Mungu kwa fursa hii tena ninapokukaribisha katika somo letu linalohusu Msamaha.

Ndugu yangu, Dhana ya Kusamehe inaweza kutafsiliwa kama hali ya kuachilia au kupuuza jambo ambalo limekugusa, limekukwaza, limekuudhi nak..... lakini wakati huo unao yhalali wa kudai fidia, au kuruhusu hukumu impate mkosefu wako yani aliekukosea.
Na uanajua pengine ungeliongea jambo hili lingeeza likazusha mjadara mkubwa, na pengine lingegusa kila mmoja wenu.namaanisha labda katika:( Familia, Jamii,Cmpuni,Kanisa,Offisini nak...............).
Aidha kwa kusamehe au kusamehewa! KWA UFUPI, GHARAMA YA MSAMAHA HUWA NI YA YULE ANAYESAMEHE, JAPO ALIETAKIWA KULIPA NI ALIESAMEHEWA.
Naomba unielewe vizuri hapa, unaposamehe, kwako huna dukuduku, ila aliyesamehewa hubaki na maswali mengi kama vile hakutegemea kusamehewa.

Hii inadhihirisha kuwa, mara unaposamehe, anayesamehewa anabaki na maswali kichwani kuwa kweli kasamehewa au laa, na hii ndiyo gharama halisi.
Kuna watu wengine husema; katu siwezi kusamehe, na hata nikisamehe siwezi kukusahau. Usipowasamehe wengine Makosa yao, kamwe hautosamehewa makosa yako. Si maneno yangu; Bibila (Mathayo 6:12)
Ni wazi kuwa kumsamehe mtu aliyekuumiza sio jambo lakawaida na wala si suala la dogo lakini hapohapo ndipo utu wako unapojidhihilisha pamoja na uvumilivu wako. 
Wengine machoni pa watu hudiriki kusema “Yameisha” mara nyingi baada ya USULUHISHO, lakini ndani ya mioyo yao bado hajasamehe.
Usichoke kusamehe, kwa kuwa neno linasema samehe saba mara sabini tena kwa kwa kutwa, tena linaongeza, usichoke kutenda wema maana kipimo utumiacho kuapimia wengine ndicho kitakachotumika kukupimia nawewe.

Naomba unielewe vizuri hapa, Hii inamaana kuwa, kwanza una kheri wewe uliyepewa ufunuo hata ukajua kuwa yule kakutendea uovu, je si kazi yako kumsamehe na ndipo uanze kumuelimisha?
Mpendwa, naomba nikwambie kuwa, kwa kusamehe, unajipatia kibali mbele za Mungu na machoni mwa watu, na kuondokewa mizigo mingi ya mawazo kwa wale wakukoseao?

Ivi Unajua magonjwa haya si lazima uwe hoi kitandani, pengine unaweza hata ukawa na hasira tu, basi wee samehe ili Mungu akuondolee hasira hiyo.
Tena ukimsamehe ongea nae vizuri, mtolee ushuhuda mzuri na mfanyie vitendo vizuri amavyo vinamudhihilishia moja kwa moja kua umemusamehe.
Nawasihi,tuepuke misamaha ya kinafiki ya kusema eti nimekusameha lakini sitakusahau,msamaha wa namna hii si msamaha wa kweli, na msamaha huu hautoki moyoni .Epuka na mizigo hiyo. Kumbuka kukaa na kinyongo moyoni kwa kumsamehe fulani kwa mdomo, uku moyoni ukiwa maswali ya kwanini huu si mzigo mdogo.
Mukisamehe nanyi mutasamehewa na kama mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi.
Haya si maneno yangu (Bibilia Isaya 1:18).  Rafiki yangu, inakuwaje wewe ukisamehe ukumbuke, ebu uache moyo wako uwe mweupe usiwe na madoamadoa, usiwe na kinyongo! 

Samehe uwekwe huru.

Usihesabu makosa bali uhesabu ni mangapi utakayoyapata uko mbeleni katika jambo kubwa sana ulolifanya la kusamehe na kusahau utukufu.
Ikiwemo; Amani ya moyo,furaha, nak...... na tukiachilia mbali thamani utakayojihisi kuanayo wewe mwenyewe, lakini pia hata watu walokuzunguka watakuona wa thamani

Hivyo nakuomba ndugu mpendwa unayesoma makala hii tuungane katika kdhihilisha jambo hili la "MSAMAHA"



Kwa leo tunaishia hapa, lakini kbla sijafunga ukulasa huu nikuombe uendelee kua nasi. Utembelee blog yetu mara kwa mara kwa makala nyingi Kama: 1Mapenzi
                                                                                     2Mahusiano
                                                                                     3Kushauliana
                                                                                     4Mijadala Mbali Mbali Y Maisha Nak........
Lakini pia kama una story yeyote usisite kutumia kupitia Email Yetu: maarifablogspot@gmail.com 

Comments

Popular posts from this blog

PAUL&SARAH SEHEMU YA KWANZA NA JUMA CHECHEKA

SARAH&PAUL sehemu ya tano

hadithi ya Paul na Sarah sehemu ya6