MANENO YENYE UHAI SIKU ZOTE HUBAKI KUA HAI



MANENO YENYE UHAI SIKU ZOTE HUBAKI KUA HAI HATA KAMA ALIEONGEA ANGEZIKWA HAI

         Vitu hivi 10 ni hatari sana na hupaswi kufanya au kurudia katika maisha yako yote:


1. Kuhifadhi Chuki Na Vinyongo.

Ukiweka chuki, roho mbaya dhidi ya mtu au watu fulani unajiumiza wewe mwenyewe na nafsi yako. Kuweka chuki moyoni mwako ni sawa na kunywa sumu ukidhani kuwa atakufa mtu mwingine. Faridi Kubanda husema hivi, "Chuki humchoma aliyeihifadhi". Chuki ni ujinga ambao huzaa uovu utakaokunyima furaha kwenye maisha yako. Samehe, sahau, kua kisha endelea na maisha yako. Kusameha na kusahau ni dalili ya utu uzima, kutokusamehe ni dalili ya utoto. Inatosha kuwa mtoto, ni wakati wa kuwa mtu mzima.

2. Jfunze Kupanga Na Kutimiza

Unapanga kufanya kitu fulani kwa muda fulani, muda huo ukifika unapanga tena kufanya muda mwingine. Unapanga kuanzisha biashara mwezi ujao, mwezi ujao ukifika huanzishi unapanga kuanzisha mwezi mwingine. Unapanga kwenda mahali fulani kesho, kesho ikifika huendi mpaka mwaka unaisha. Hii sio hatari ndogo ni hatari kubwa mno. Unaweza ukazeeka unapanga tu bila kufanya na hii ndio huleta tofauti kati ya masikini na watu waliofanikiwa. Watu waliofanikiwa hupanga na kufanya. Masikini hupanga bila kufanya.

3. Kujilinganisha na watu wengine
.
Jikubali wewe mwenyewe, jiamini, ona kwamba unaweza. Ukijkubali wewe ndipo watu wengine watakukubali. Pia kujilinganisha na watu wengine ni kujinyima furaha. Kila mtu alizaliwa akiwa wa pekee na wa tofauti kwa hiyo hata ufanyeje wewe utaendelea kuwa wewe na yule ataendelea kuwa yule. Upekee ni uzuri, utofauti ni nguvu. Jivunie kuwa wewe na sio mtu mwingine.

4. Starehe & Anasa Kupitiliza.

Utumiaji wa pombe, sigara, madawa ya kulevya. Ngono, hivi ni vitu ambavyo huweza kukufanya sio uwe masikini tu bali ufe masikini. Anasa, starehe ni dhambi na mshahara wa dhambi ni........... Badilika, achana ma tabia chafu, pia mshauri na mwenzio kuacha haya mambo. "Maisha ni kama mshumaa uwakao kwenye upepo uvumao sana, usipoyalinda unayapoteza. Linda maisha yako".

5. Kupinga Uongo Dhidi Ukweri

Sisemi tusiwe wadadisi au tusiulize maswali au tusitafiti mambo kwa mapana zaidi, hapana. Nachotaka kusema ni kwamba, hata kama umejaliwa uwezo wa kubadilisha uongo kuwa ukweli na watu wakakubali hilo sio jambo la kujivunia sana. Wajuaji wako wengi sana na ubishi wa sifa wakati mwingine haufai. Usimbishie mtu eti tu kwa sababu unamzidi umri, eti tu kwa sababu unamzidi cheo au elimu au nguvu, ni vibaya sana. Hili ni kosa kubwa sana. "Ukweli unaweza ukautupa motoni na usiungue". Hata ufanyeje hutaweza kuuficha ukweli kama ambavyo huwezi kulificha jua.

7. Uvivu & Uzembe.

Ukitaka kuwa masikini, ukitaka kufa masikini ni rahisi sana. Kuwa mvivu, kuwa mzembe. Sikuwahi kuona wala kusikia mtu mvivu, mtu mzembe mwenye mafanikio ya maana. Thomas A. Edson, mgunduzi wa bulb, alikuwa akilala masaa manne tu, Paul Mashauri, mhamasishaji kutoka Tanzania huwa anaamka saa kumi na nusu alfajiri kila siku. Aliko Dangote, tangu mwaka 1978 mpaka leo anafanya kazi masaa zaidi ya 16 kila siku, P. Did, mwanahiphop tajiri namba moja duniani aliwahi kuwa anafanya kazi masaa 17 kila siku. Uvivu ni ujinga uletao umasikini katika maisha.

8. jibu La Ndiyo Kwa Kila Jambo

Ukiwa mtu wa ndiyondiyo kwa kila kitu jiandae kukosa kila kitu. Watu wanaosema ndiyo kwa kila kitu hukosa kila kitu.Unachohitaji ni msimamo na kulinda heshima yako wewe kama binadamu. Usifanye kila kitu kwa sababu fulani anafanya, Jifunze kusema hapana kwa lile jambo ambalo unaona sio sawa kwako au kwa wengine. Usiishi ndani ya mawazo ya mtu mwingine maana maisha ni mafupi Sana, sikiliza moyo wako fuata moyo wako kisha tumia akili yako ipavyo.

9. Kuogopa Kushindwa.

Kuogopa kushidwa ni kiggezo cha kushindwa. Na uthubutu ni kigezo cha kujiamini. na kujiamini ni kigezo cha ushindi. kuogopa kushindwa ni kikwazo kikubwa sana katika maisha ya kiutu uzima. Jay Z anasema kwamba, "siogopi kufa, ila naogopa kutokujaribu". Fanya ushindwe, lakini usiamini katika kushindwa, ila kushinda. "The only war won or lost, can be described" ~Nelson Mandela.

10. Kutokujifunza.

Kadri unavyojifunza ndivyo unavyojua jinsi gani hujui. Tatizo sio gharama ya Kitabu, tatizo ni gharama utakayolipa baada ya kutokusoma hicho kitabu. Sisi ni matokeo ya vile tunavyojifunza kwa hiyo kama hujifunzi wewe sio chochote.

Popular posts from this blog

PAUL&SARAH SEHEMU YA KWANZA NA JUMA CHECHEKA

SARAH&PAUL sehemu ya tano

hadithi ya Paul na Sarah sehemu ya6