UKWELI UKO WAPI? sehemu ya kwanza
UKWELI HUMUINUA MTU KUTOKA CHINI MPAKA JUU .
UKWELI NDIO NJIA PEKEE IKAYOKUFANYA UISHI UKIWA HURU MAISHA YAKO YOTE.
UKWELI UTAKUFANYA UWE MUAMINIFU KATAKA JAMII,
FAMILIA,KAZINI,DARASANI NA KWINGINEKO.
HIVYO UKWELI HUU UTAYABADILI MAISHA YAKO KUA YENYE FURAHA SIKU ZOTE.
ZAIDI FUATILIA KISA HIKI APA CHINI
Alipofikia umri wa pale mtu aanzapo kujitambua, Kijana huyu aliendelea na masomo yake uku akiwa tayari alishaunganishwa na kampuni alipokua akiidhinisha kwa vitendo kile anachokisoma chuoni. Kampuni yao ilifanya mpango ili yeye na wanafunzi wenzake kadhaa wazoezwe kwa siku mbili kwa week na mda huu ulikua ni mda ambao upo nje ya siku za kwenda katika chuo alichokua akisoma. Siku moja, walimaliza masomo mapema kuliko ilivyokuwa kawaida, kulingana na latiba ya chuo icho. Aidha kulingana na sheria za kampuni iliowapa nafasi hizi, siku moja wanafuzi hawa walimaliza kazi waliokua wamepewa, kabla ya mda uliopangwa. Wanafunzi hao walipaswa kubaki na kuendelea na kazi zingine hadi mwisho wa siku, kwa mjibu wa kampuni hio. Badala yake, wanafunzi wengine wote walienda kujifurahisha, lakini "Kijana" huyu akabaki kazini. Na Katika hali amboya hakuitarajia :Kijana huyu, mkurugenzi wa kampuni aliyekua akiwasimamia wanafunzi hao akaja. Alipomwona, "Kijana huyo alimuuliza hivi: “Mbona hukwenda darasani leo? Na wanafunzi wenzako wako wapi?” "Kijana huyu alipaswa kutoa jibu gani?
Watu wengi wanajikuta katika hali kama ya Ndugu yetu huyu. Je, angesema ukweli ili yeye aonekane bora kwa mukurungenzi wao? au angesema uwongo ili kuwalinda wanafunzi wenzake? Kusema ukweli kungewaletea wenzake taabu. Je, ni sawa kusema uwongo katika hali kama hii? Wewe ungefanya nini?
Kisa hiki kitaendelea siku chache zijajo, wewe chakufanya ni kutemblea blog yetu mara kwa mara.
Kisa hiki kitaendelea siku chache zijajo, wewe chakufanya ni kutemblea blog yetu mara kwa mara.
Tuma Email:maarifablogspot@gmail.com
au weka comment yako apo chini
au weka comment yako apo chini
Kumbuka maoni yako ni funzo kwa wengine
